Monday, August 2, 2010

Phasing out support for older browsers

Phasing out support for older browsers

Kijiji cha Malangali wilayani Mufindi mkoani Iringa


Jiwe hili ni kivutio kwa witalii hapa nyoka wenye sumu wanapatika eneo hili tena wa jeuri picha na Daudi Mwangosi

Daudi mwangosi wa pili kutoka kulia ,akiwa na watumishi wa halimshauri ya Njombe katika jiwe lilichongwa lenye sura ya ramani ya bara la Afrika.Linapatikana huyo Njombe

Daudi mwangosi akiwa moja ya eneo la mvuke wa maji ambapo vyura wanazaliana huko kihansi Ifakara mlimba mkoani morogoro

Daudi mwangosi -kihansi


Daudi mwangosi akijandaa kupanda milima kuelekea kwenye maporoko ya maanguko ya maji wanako zaliana vyura jamii ya pekee

Daudi mwangosi -kihansi


Friday, July 2, 2010



Nikufa na kupona lakini usalama wa Raia na mali zao ukjo mikononi mwetu


Askari ni Askari tu


Hatuna jinsi


Usijali ni maisha tu


Wakzi wa kijiji huu ndiyo usafiri wao


Askali wa mwema


IGP Akipokea heshima ya kijeshi kwa kamnda wake wa kikosi cha kutuliza ghasia


Askari mkoani Iringa wakiwa maoja ya mazoezi ya kumpokea IGP


IGP Said Mwema na mwenyeji wake Kmanda wa polisi mkoa wa Iringa Evaristo Mangala


Afande IGP Mwema katika ziara yake mkoani Iringa aliwahi kuulizwa swali lifuatalo;-Afande IGP huoni kuna changamoto kubwa inayolikabili jeshi lako tangu kuanzishwa kwa falsafa ya polisi jamii
-Hivi karibuni tumeshuhudia kuibuka vitendo vya kulidhalilisha jeshi lako pale wananchi wenye hasira kali kuvamia vituo vya polisi na kuwapiga watuhumiwa hadi kuwa ua.
-Je kuna mtazamo gani kwa siku za usoni kuhusu kukabiliana na changamotohiyoambayo inaifedhehesha dola ,Iko falsafa isemayo tazama ulipojikwa ,sio pale ulipoangukia ?














Ng'ombe na Mbuzi-katika mahusiano ya kawaida



Wanyama pia wanautashi tofauti na binadamu anavyowafikiria ,wanyama hawa ng'ombe na mbuzi ni jamii mbili tofauti hata hivyo wanaheshimu hali zao ,hawabaguani kwa misingi ya utofauti walio nao kwa misingi ya kuzaliwa kwao.

Miji ya vijiji vyetu ninani mwenye jukumu la kuiboresha ili upande kutoka kwenye hali ya uduni iliyonayo kwa sasa na kuwa katika hali ya ubora ,pengine tunataka makazi haya ya hifadhiwe kama makumbusho kwa siku za usoni?

Hali hii itaendelea hadi lini , watanzania hawa utafikiri wakimbizi katika nchi yao , kijiji hiki hakiko mwendo mrefu kutoka Iringa mjini , serikali imeendelea kuwaahidi wananchi hao kwamba itaafikishia huduma hiyo ya maji, baadala yake serikali itegemea mhisani wa shirika la dini la Rome bila kuzingatia kuwa mhisani huyo jambo lolote linaweza kutokea aidha kuahirisha maamuzi yake .

Wakazi wa kijiji cha kising'a wilayani Iringa


Hii ni foleni ya wakazi wa kijiji cha kising'a wakisubiria kukinga maji kwenye bomba ambayo inatoa maji kidogo ,wakazi hao wamekuwa wakipata adha ya mateso ya kuamauka usiku wa manane kufuata maji ,hata wakati mwingine wanagombana wao kwa wao ,pamoja na hayo wanahoji serikali yao iko wapi kuwatatulia kero hiyo ambayo imekuwa ikiwasibu miongo hadi miongo.

Saturday, June 26, 2010




Toadina kinyaga mjane mkazi wa mkungugu ;anaelezalicha ya kuwepo kwa ukame katika eneo hilo ,kuna matatizo mengine mwambata yanayochangia wakazi hao kukosa chakula cha uhakika.


Anabaisha tatizo la kwanza kuwa ni zana duni zxa kilimo wanazotumia mashamba yao wanapoandaa hawamalizi kwa wakati hujikuta msimu umepita,


Uwezo mdogo wa kifedha kwa ajili ya kunulia pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea ya luzuku amabayo ameshindwa kumudu kutokana na gharama yake kuwa kubwa kiasi cha sh54000/=kwa mfuko mmoja.



Picha za wakazi wa mkungugu






Wakazi wa Mkungugu katika jimbo la ismani wilayani Iringa mkoani humo hali ni tete kutokana na njaa kali inayo waandama,baada ya kushindwa kuvuna mazao kutokana na ukame ,mvua ilikatika mapema ingawa hivi karibuni serikali ilitoa chakula cha msaada kwa wahanga hao hakikutosha.kama picha hii bi evelinakivike na mwanaye Juliana Luhala wakisaidiana kuokota punje za mahindi .