Saturday, June 26, 2010




Toadina kinyaga mjane mkazi wa mkungugu ;anaelezalicha ya kuwepo kwa ukame katika eneo hilo ,kuna matatizo mengine mwambata yanayochangia wakazi hao kukosa chakula cha uhakika.


Anabaisha tatizo la kwanza kuwa ni zana duni zxa kilimo wanazotumia mashamba yao wanapoandaa hawamalizi kwa wakati hujikuta msimu umepita,


Uwezo mdogo wa kifedha kwa ajili ya kunulia pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea ya luzuku amabayo ameshindwa kumudu kutokana na gharama yake kuwa kubwa kiasi cha sh54000/=kwa mfuko mmoja.



Picha za wakazi wa mkungugu






Wakazi wa Mkungugu katika jimbo la ismani wilayani Iringa mkoani humo hali ni tete kutokana na njaa kali inayo waandama,baada ya kushindwa kuvuna mazao kutokana na ukame ,mvua ilikatika mapema ingawa hivi karibuni serikali ilitoa chakula cha msaada kwa wahanga hao hakikutosha.kama picha hii bi evelinakivike na mwanaye Juliana Luhala wakisaidiana kuokota punje za mahindi .